GET /api/v0.1/hansard/entries/1066986/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1066986,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066986/?format=api",
    "text_counter": 82,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
    "speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
    "speaker": null,
    "content": "Ndungu zangu Wabunge, rai yangu kwenu ni kuomba mtusaidie kulea uhusiano wetu mzuri. Ninasema hivyo nikitambua kwamba nyinyi ndio wawakilishi na sauti ya wananchi wa Kenya. Nyinyi ndio wenye dhamana ya kutunga sheria na kushauri Serikali juu ya mwelekeo wa sera na kuongoza wananchi wenu waliowachagua. Dhima yenu katika kukuza ushirikiano baina ya nchi zetu mbili ni kubwa sana. Mnao uwezo mkubwa wa kuamua kasi ya ushirikiano wetu iwe ya haraka ama ya kusuasua kwa aina ya sheria mtakazotunga na sera mtakazopitisha. Dira na mwelekeo wa Serikali ya awamu ya sita ninayoiongoza ni kudumisha mazuri ya awamu zilizopita, kuyaendeleza mema yaliyoko na kuleta mazuri mengine mapya. Nimekuja kuwaahidi kuwa chini ya uongozi wangu, mimi na wenzangu katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tutafanya kila linalowezekana kuimarisha uhusiano kati ya nchi zetu mbili. Kama kuna jambo linalolegalega au kama uhusiano wetu unasuasua, basi nimekuja hapa Kenya ili kukazia yale ambayo yamelegalega. Nimekuja kuyanyoosha yale ambayo yalikuwa yamejipindapinda. Leo mtasoma Kiswahili."
}