GET /api/v0.1/hansard/entries/1066993/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1066993,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066993/?format=api",
    "text_counter": 89,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
    "speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
    "speaker": null,
    "content": "Daima, tuwatangulie wafanyabiashara na wananchi wetu katika utangamano na kuwaongoza badala ya wao wananchi wetu kutuongoza sisi. Yanayotokea sasa hivi ni kwamba wafanya biashara wako mbele kuliko sisi. Inabidi sasa tutunge sera na sheria kuendana na mwenendo wa wafanya biashara. Lakini inavyotakiwa, ni tutunge sera na sheria ili wafanya biashara wafuate sera na sheria zetu. Nasema hayo kwa sababu falsafa zinasema kuongoza ni kuonyesha njia na sio kufunga njia. Sisi kama viongozi wa serikali, mabunge na mahakama zetu tunapaswa kuonyesha wananchi wetu nji na tusiwafungie njia za maendeleo au ustawi wao."
}