GET /api/v0.1/hansard/entries/1066995/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066995,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066995/?format=api",
"text_counter": 91,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
"speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
"speaker": null,
"content": "Waheshimiwa Maspika, Maseneta na Wabunge wa Bunge la Taifa, nitimishe hotuba yangu kwa kusema kwamba kama mnavyojua, moyo ukilemewa na furaha, furaha ya moyoni hutoka mdomoni. Ningetamani kuendelea kuzungumza nanyi kwa kirefu zaidi, kueleza furaha yangu kwa upendo mkubwa mlionionyesha, ukarimu mkubwa mliotufanyia mimi na ujumbe wangu na heshima kubwa mlionipa. Isitoshe, tunapokutana Tanzania na Kenya, tunakuwa na maneno mengi sana ya kuzungumza, hayaishi. Hii ni kutokana na ukubwa na uzito wa uhusiano wa nchi zetu mbili. Sitaki kusema naishia hapa bali mniruhusu ni ahirishe maneno yangu hapa."
}