GET /api/v0.1/hansard/entries/1067153/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1067153,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1067153/?format=api",
    "text_counter": 147,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Samburu CWR, KANU",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Maison Leshoomo",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": " Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Naomba kusema kuwa mimi ni mmoja wa wanakamati wa BBI. Ingekuwa muhimu kama wenzangu wangekuwa hapa kunisikiliza na kuelewa kile tumepata kutoka Kaunti 47. Kama Rais Uhuru na Waziri Mkuu wa zamani, Mhe. Raila Odinga, hawangechukua jukumu la kuelewana, nchi hii ingekuwa na matatizo mengi sana. Lakini walikubaliana na tukapewa jukumu la kuzitembelea kaunti 47 kuchukua maoni ya wananchi. Viongozi wa Kenya wako kule mashinani pia. Tunasema hivyo kwa sababu haya maoni ambayo yako katika BBI ni ya wananchi. Kile wananchi walitamuka ndicho kiko katika BBI. Hakuna watu walioenda kujitengenezea maoni yao katika BBI. Ningependa kuwaambia wenzangu kama wangekuwa hapa waunge BBI mkono tena sana. Hii ni kwa sababu tunataka wananchi wapate handshake . Kama tulikuwa tunapigana ama kuzozana, tumesahau kwa sababu ya handshake ."
}