GET /api/v0.1/hansard/entries/1067155/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1067155,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1067155/?format=api",
"text_counter": 149,
"type": "speech",
"speaker_name": "Samburu CWR, KANU",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Maison Leshoomo",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Wananchi walisema wanataka Mbunge wa Bunge la Kaunti (MCA) awe na keki yake ndiyo wamuulize maswali kwa sababu wanaketi naye huko mashinani. Sisi tuko Nairobi na yule MCA aliyechaguliwa mashinani wanataka awe na keki yake huko, na haya ndiyo maoni yao. Wananchi walisema wanataka Waziri wa Serikali Kuu atoke ndani ya hii Nyumba yetu. Hayo sio maoni ya wakubwa, lakini ni ya wananchi. Kama ningekuwa na nafasi ya kuongea, ningewaelezea wenzangu maoni mengi ya wananchi. Ukija hapa kusema unapinga, jua unapinga wananchi sio sisi. Wenzangu, ningetaka kusema kwamba tumeona wananchi wako na macho. Unajua kama kitu ni kizuri na unataka kukipinga, utakipinga hata kama ni kizuri. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}