GET /api/v0.1/hansard/entries/1067633/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1067633,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1067633/?format=api",
"text_counter": 153,
"type": "speech",
"speaker_name": "Samburu CWR, KANU",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Maison Leshoomo",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": " Asante sana Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii pia mimi nichangie mambo haya ya BBI. Ninashukuru kwa sababu jana sisi ndio tulifunga Bunge tukingoja kuzungumza. Ningependa tu kusema yale mambo niliyoyabakisha jana. Nikisimama hapa ninasimama kama Mheshimiwa wa Samburu County na pia Memba wa Kamati ya BBI. Kwa hivyo, ninaweza kuzungumza. Tafadhali niseme kile nimeona. Mhe. Naibu Spika, mimi ni mmoja wa wale walizunguka kaunti 47. Nataka niwaambie machache Wajumbe wenzangu. Wakati tulikuwa tunatembea katika kaunti 47, maoni kuhusu BBI, tuligundua kuwa siyo ya wakubwa na siyo ya yeyote. Ni ya mwananchi. Mwananchi ametupatia maoni tofauti tofauti. Naibu Spika, ningependa kusema machache tu. Tulipewa ajenda tisa na Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga. Maoni hayo yalikuwa ya kuuliza wananchi kueleza maono yao juu ya Kenya. Maoni hayo pia yalikuwa yaeleze Wakenya jambo la vita kila wakati tunapofanya uchaguzi. Kwa sababu ya muda, ningependa kusema kuwa wananchi walitoa maoni yao. Ningependa kuomba wenzangu waniskize kwa makini. Kwanza, walisema kuwa mambo ya siasa yanapiganiwa wakati wa uchaguzi wa urais na wala sio wakati wa uchaguzi wa magavana au Wabunge. Waliomba kuwa ikiwezekana viti vya juu vigawanywe vitoshe kila mtu ili tusiwe na vita hivyo. Wananchi walitoa maoni yao kuwa na viti vya Waziri Mkuu na naibu wake. Ningependa kueleza kuwa wawakilishi wa wadi wetu hawakupitisha BBI kwa sababu ya hiari yao lakini kwa sababu ya amri ya wananchi. Tulipokuwa tukizuru kaunti mbalimbali tulikuwa na wawakilishi wadi ndio maana walipitisha BBI kwa sababu walisikia maoni ya wananchi wao. Wananchi walisema kuwa kaunti na maeneo Bunge yasiguswe. Na pia wawakilishi wadi waangaliwe kwa sababu ndio wako mashinani. Ningependa kuwaambia wenzangu kuwa mambo ya BBI ni ya wananchi na wala sio ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga. Anayekataa kuunga BBI mkono amekataa maoni ya wananchi. Wananchi walitoa maoni yao na walituambia kuwa tangu uhuru, hawajawahi kuulizwa maono yao juu ya Kenya. Wananchi walifurahia “handshake” ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga hadi wale ambao hawasikizani walianza kuongea. Ningependa kurudia kusema kuwa BBI ni maoni ya mwananchi. Tulipokuwa tunazuru nchi, wenzangu hapa walikuwa wanakataa BBI lakini ni vizuri wakumbuke kuwa hii ni maoni ya wananchi. Tupitishe BBI kwa sababu ni maoni ya wananchi. Naibu Spika, wananchi walisema kuwa mawaziri wachaguliwe kutoka Bungeni kwa sababu Mbunge wake akipewa kiti hicho atakuwa katika Serikali ya Kitaifa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}