GET /api/v0.1/hansard/entries/1067665/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1067665,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1067665/?format=api",
    "text_counter": 185,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "zilifanya tupoteze Wakenya wengi. Pia hapa Kenya tulikuwa na ukabila mwingi sana na kumekuwa na ufisadi ambao umekidhiri. Mswada huu unazungumzia mikakati ya kuweza kupambana na ufisadi, vipi tutaweka usawa katika taifa letu, umoja na pia kuweka uzalendo? Lakini haswa kabisa Mswada huu umezungumzia vipi tutapata huduma mashinani. Wakati tunazungumzia ugatuzi mashinani lazima pia tuzungumzie fedha mashinani. Hivyo basi, iwapo asimilia 35 itakuja mashinani, itamaanisha tutaweza kupata huduma sambamba na zile fedha zitakuja mashinani. Vile vile, zile fedha ambazo zitakuja katika wadi zitakuwa fedha ambazo zitasaidia wadi zetu kuweza kupata miradi, hata kama yule Mjumbe wa Kaunti atakuwa haskizani na gavana, pengine hawatoki chama kimoja ama walikosana katika mambo ya uchaguzi, bado watu wa sehemu hiyo ya wadi wataweza kupata miradi yao bila kubabaishwa na jambo lolote. Mswada huu pia umezungumzia pesa za kusawazisha, ambazo kwa Kiingereza tunaita"
}