GET /api/v0.1/hansard/entries/1067667/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1067667,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1067667/?format=api",
"text_counter": 187,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": ". Imesema pesa hizi za kusawazisha zitaongezewa miaka kutoka 20 hadi 30. Pesa hizi zitasaidia sehemu zilizotengwa kama kaskazini mashariki, pwani na sehemu zingine katika Jamhuri yetu ya Kenya ambazo zilitengwa katika miradi kama mambo ya barabara, maji na afya. Kwa hivyo, Mswada huu umezungumzia mambo mazuri ambayo yatasaidia taifa hili. Pia, umezungumzia vipi akina mama wataboreshwa katika nyanja za uongozi na maamuzi. Hivyo basi, katika Seneti kina mama 47 watakuwa na nafasi ya kutoa maamuzi na kuangalia zile fedha katika kaunti zetu, kutoka kwa ngazi za juu katika taifa letu na hata zile ambazo kauti zimeweza kukusanya pale mashinani. Kina mama watakuwa na sauti na wanaweza kupiga kura na kufanya maamuzi. Vile vile, pia uongozi utakuwa wa akina baba na mama sambamba, sako kwa bako iwapo gavana ni mwanamke, basi naibu wake atakuwa mwanaume. Iwapo ni mwanaume naibu atakuwa mwanamke. Sasa hivi tunaona Magufuli aliweka naibu mama Suluhu na tunaona ambavyo amejizatiti na kuweza kuongoza taifa la Tanzania kwa njia safi tena sana. Vile vile, pia Mswada huu umezungumzia tume ya vijana ambayo itawakilishwa na vijana wa kike na kiume katika njia ya usawa. Tume hii itaweza kuangalia mipango ya vijana, ratiba na sera ambazo zitazungumzia matatizo, maendeleo na vile kuboresha hali ya vijana ili kuwawezesha katika miradi ya maendeleo. Vile vile, vijana wataweza kupata mapumziko kutokana na ulipaji wa ushuru katika biashara zao kwa muda wa miaka saba. Hili ni jambo ambalo litaweza kukuza vijana katika mambo ya vipawa, miradi ya biashara ndogo ndogo na ile mikubwa kwa wale watakuwa wamepata uwezo. Mswada huu umezungumzia ile sheria ya thuluthi-mbili ya jinsia vile itaangaliwa. Hivi sasa hatutakuwa na kizungumkuti na utata katika kujua je, hii sheria ya jinsia itatekelezwa kwa njia ngani? Itatekelezwa kwa njia ambayo Mswada huu umezungumzia. Mswada huu pia umezungumzia kuwa tutakuwa na mawaziri watakaoteuliwa miongoni mwa Wabunge waliochaguliwa katika maeneo Bunge. Hivyo basi, iwapo tuna mswali ya kuzungumzia, mambo ya sehemu zetu ambazo tunawakilisha tutauliza hapa katika Bunge. Waziri atakuwa hapa na ataweza kukupatia jawabu. Si kama sasa ambako lazima utoe taarifa kwamba unataka Waziri fulani aje umuulize maswali haya. Waziri naye anajibu kwamba atapatikana ama hatapatikana. Kwa hivyo, tutakuwa na wakati mwafaka wa kuweza kuwauliza maswali mumu humu Bungeni. Mswada huu pia umetupatia nguvu kiasi kwamba fedha za NG-CDF ambazo zinakuja katika eneo bunge zitawekwa katika Katiba. Hivyo basi wale wakereketwa ambao wamezoea kupinga matumizi ya pesa hizo ambazo zimemsaidia mlalahoi na yule maskini pale mashinani... Fedha hizi zitajulikana tu sawia na zile pesa ambazo zinaenda kwenye kaunti. Zitakuwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}