GET /api/v0.1/hansard/entries/1067671/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1067671,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1067671/?format=api",
    "text_counter": 191,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": " Mhe. Naibu Spika, hata maseneta sasa hivi watakuwa na uwezo wa kuangazia zile fedha ambazo zimekusanywa na kaunti na si zile tu ambazo zimetoka katika ngazi ya kitaifa. Vilevile watu watateuliwa baada ya kura kupigwa na watu kuchaguliwa. Watakaoteuliwa ni wale ambao pia wamegombea na kung’ang’ana katika uchaguzi na pengine kwa bahati mbaya au nzuri wakaanguka. Wao ndio watapatiwa nafasi. Mhe. Spika, naunga mkono Mswada huu kwa sababu ni Mswada ambao utaleta maridhiano na maelewano katika taifa. Mambo ya uchaguzi yatakuwa na imani na kutakuwa na amani katika taifa letu la Kenya. Asante, Mhe. Spika."
}