GET /api/v0.1/hansard/entries/1067806/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1067806,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1067806/?format=api",
    "text_counter": 326,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ruiru, JP",
    "speaker_title": "Hon. Simon King’ara",
    "speaker": {
        "id": 13468,
        "legal_name": "Simon Nganga Kingara",
        "slug": "simon-nganga-kingara-2"
    },
    "content": "Nikigusia jambo hilo, ningetaka kutambua kuwa Eneo Bunge la Ruiru ambalo ninawakilisha saa hii liko na idadi ya watu 600,000. Mwaka wa 2019, eneo Bunge hilo lilikuwa na watu 490,000 na eneo Bunge hilo liko na watu wengi kuliko zaidi ya kaunti sita ambazo nitataja. Hata hivyo, mapato huwa ninapewa kama Mbunge wa eneo Bunge linguine. Kaunti ya Samburu ina watu 300,000. Kaunti ya Tana River ina watu 300,000. Kaunti ya Taita Taveta ina watu 340,000. Kaunti ya Tharaka-Nithi ina watu 393,000 na Kaunti ya Lamu ina watu 140,000, lakini Ruiru ambalo ni eneo Bunge, lina watu 490,000. Hata hivyo, mapato ambayo ninapewa hapa ni sawa na yale maeneo Bunge ambayo yako katika kaunti hizo ambazo nimetaja na ziko na Wabunge tatu kuenda juu katika kila kaunti."
}