GET /api/v0.1/hansard/entries/1067812/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1067812,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1067812/?format=api",
    "text_counter": 332,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ruiru, JP",
    "speaker_title": "Hon. Simon King’ara",
    "speaker": {
        "id": 13468,
        "legal_name": "Simon Nganga Kingara",
        "slug": "simon-nganga-kingara-2"
    },
    "content": "Jambo lingine ningegusia linahusu usawa wa Independent Electoral and Boundary Commission (IEBC). Ukiangalia katika utaratibu na pendekezo la IEBC, Mbunge mmoja anatakiwa kusimamia watu 133,000. Kwa hivyo, wakati unapopata suluhu ya kugawa Ruiru kwa vipande kama vitatu ili niache kuwakilisha watu 600,000 ili niwakilishe watu 160,000, ingekuwa sawa. Kwa hivyo, sioni ni kwa nini watu hawaoni haja ya kuunga mkono Mswada huu. Vilevile, ukiangalia kama sasa na watu wako wengi namna ile na rasilimali ni kidogo, hospitali, shule, usalama na pesa za barabara ni duni halafu tunalalamika na sisi ndio tumekataa kuweka mikakati mwafaka itakayoweza kuleta uwiano katika maendeleo ya maeneo Bunge. Inaweza kuwa wawili-watatu walisema jambo la kusita na la kuumiza. Lakini, tuangalie mbali tuone ni wapi mwananchi atapata haki yake. Katika utaratibu ule, kuna jambo lingine la maana sana la kupeleka pesa zaidi katika serikali gatuzi zetu. Kama pesa zitaenda mashinani, nimesema zitaambatana na maendeleo. Rasilimali zitafikia Wakenya wote na usawa na uwiano utapatikana katika maendeleo. Vilevile, kuna pale pamegusiwa kuangalia maneno ya jinsia."
}