GET /api/v0.1/hansard/entries/1067931/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1067931,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1067931/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu East, JP",
"speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": " Ahsante, Mhe. Spika. Nataka nichukue fursa hii kuungana na wenzangu ambao wametangulia kuzungumza kwa kupinga na kukataa marekebisho haya. Vile vile, nataka niseme kwamba nchi hii inawashukuru pakubwa Mhe. Raila Odinga na Mhe. Uhuru Kenyatta kwa kunyamazisha fujo iliyokuweko nchini. Miongoni mwa fujo hizo tulikuwa sisi viongozi. Leo hii nchi inashuhudia kwamba hakuna tena makelele na matusi. Tunalolijadili mbele yetu ni suala la uchumi na mazingira ama miundo msingi katika nchi yetu ya Kenya. Tunayajadili haya yote yaliyoko mbele yetu kama Wabunge tuliopewa fursa. Ni mambo mazuri tunapoyaona na kuyasoma lakini yote yanahitaji kutekelezwa baada ya kupitishwa na Bunge. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}