GET /api/v0.1/hansard/entries/1067932/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1067932,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1067932/?format=api",
    "text_counter": 99,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Kwa mtazamo wangu, nikiwa kama Mkenya na kiongozi anayeishi katika hii nchi, haya yote yatahitaji fedha ili kuendelezwa. Kwa mfano, iwapo twapanga kuongeza maeneo bunge sabini, ni lazima kuwe na fedha zitakazoendesha maeneo bunge hayo. Vile vile, sote twajua na kufahamu namna uchumi wa nchi hii ulivyo. Mwisho wa haya yote, mimi na wengine tutalazimika kutoa ushuru wa ziada ilhali tunauelewa uchumi ambao tuko nao. Hakuna kiongozi atakayekataa mazuri yaliyoko katika marekebisho haya. Hofu yangu kubwa ninayotaka wakenya waifahamu ni utekelezaji wa haya mazuri tunayoyajadili yatakapopitishwa. Tunavyojua sasa ni kwamba nchi imekumbwa na madeni chungu nzima. Lazima hatua za ziada za kuhakikisha kuwa ushuru umeweza kupatikana ili kuyatekeleza haya. Ninasimama kupinga kikamilifu haya marekebisho kwa hofu kwamba huu ni mzigo ambao utaenda kwa wananchi baada ya marekebisho hayo. Kwa hayo machache, asante."
}