GET /api/v0.1/hansard/entries/1067963/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1067963,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1067963/?format=api",
"text_counter": 130,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": {
"id": 13287,
"legal_name": "Kassim Sawa Tandaza",
"slug": "kassim-sawa-tandaza"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Spika. Kwa kawaida nikisimama kwa Mswada kama huu huwa naunga mkono. Lakini kulingana na umuhimu wa Mswada huu wa leo, sitaunga mkono peke yake lakini nitaongeza na kuunga na miguu yangu yote miwili. Hii ni kwa sababu huu Mswada ukishapita na naomba tuweze kuupitisha ili uweze kutekelezwa ndio uondoe ndonda sugu sana kwa Kenya nzima na haswa watu wa Matuga na Kwale County kwa jumla. Kutoka tuanze mchakato wa vyama vingi, kila kura huwa na machafuko na kwa bahati mbaya machafuko yote huanzia sehemu za Pwani, Kwale na hususwa katika eneo bunge langu. Tukikumbuka mara ya kwanza tulipokuwa na vile vita vya Likoni ambayo imeshikana na Matuga The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}