GET /api/v0.1/hansard/entries/1067965/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1067965,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1067965/?format=api",
"text_counter": 132,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": {
"id": 13287,
"legal_name": "Kassim Sawa Tandaza",
"slug": "kassim-sawa-tandaza"
},
"content": "pale Mwambeni na Kitenge na watu wengi walioumia walikuwa wa Eneo Bunge la Matuga. Kisha baadaye kukakuja machafuko ambayo yalijulikana ulimwengu mzima ya Mbombo ambayo iko kama kilomita sita peke yake kutoka pale naishi ikiwa katikati ya maeneo ya eneo Bunge la Matuga. Kwa hivyo, ikiwa kutakuwa na hali iname yoyote ambayo itaweza kuondoa machafuko baada ya kura, basi hili ni jambo ambalo kama nilivyo tanguliza sio la kuunga mkono peke yake lakini linastahili kuongezewa na miguu. Tunajua kwamba fujo hutokea kwa sababu ya vile kura zinavyopigwa katika nchi hii. Tunapiga kura zetu kikabila na ukilinganisha yale makabila makubwa na yale madogo ambayo mara nyingi huwa mirengo tofauti, kura zao huwa zinakaribiana. Hali ni tofauti katika nchi jirani hapa ambapo watu hupiga kura kwa kufuata maadili na mienendo ya vyama. Kwa hivyo, kule huwa hakuna matatizo lakini hapa kwetu sioni kwamba itabadilika hivi karibuni kwa sababu bado, kwa bahati mbaya maana sio bahati nzuri na sio jambo la kujivunia, tunapiga kura zetu kikabila na lazima tuwe na njia mbadala ya kuona kwamba hata ikiwa tutapiga kiukabila lakini hakutakuwa na machafuko. Katiba hii ambayo tunaizungumzia saa hii kuibadilisha ni Katiba ambayo wale wanaopinga mabadiliko haya ni wale wale ambao walipinga hata hii Katiba ambayo saa hii tuko nayo. Nashangaa kwa sababu kule Pwani huwa na watu ambao tunawaita vishipa. Mtu kishipa ni yule ambaye hupinga jambo bila sababu ya maana. Kwa hivyo, ikiwa ni mpwani huwa ni kama ambaye tumemzoea lakini kwa mchakato huu, naona mpaka wenzetu wa bara wamejiunga na wale vishipa wanaopinga jambo lakini ukiwauliza sababu na maana, ukweli ni kwamba hakuna. Huwezi kupinga pesa zisiende mashinani ilhali unasema unataka yule mwananchi wa kawaida aweze kunufaika na unapinga pesa ambazo zinaongezwa kwenda mashinani. Ni jambo la kushangaza kwamba baadhi yao hata wanawania viti vya ugavana tunapoenda 2022. Wamesema kwamba wanawania viti hivyo lakini kwa hivi sasa wanapinga pesa zisiende na hali wao wenyewe wanataka kwenda kusimamia viti hivi. Pengine wamejua kwamba hawatapita ndio maana wanapinga lakini ukweli sisi watu wa Pwani kuanzia wanasiasa wetu wakongwe wakati wa marehemu Ronald Ngala tulikuwa tunataka majimbo. Majimbo ni kuletewa fedha ili tuweze kujisimamia kwa sababu tunajua moja kwa moja zile zinazobaki kule juu huwa hazitufikii. Njia moja peke yake ambayo inaweza kutusaidia ni kwamba pesa ziende kule kwa sababu hatuna namna nyingine. Hatudhani. Hata tukiwa na mawaziri wakuu watano na manaibu wao sio ukweli kwamba mmoja wao atatoka katika zile sehemu ambazo sisi tumetengwa kwa muda mrefu. Kwa hivyo, matumaini yetu ni zile pesa ambazo zitafika. Tuna matatizo ya kijadi na katika hii BBI tunajua kwamba zile pesa za Equalisation Fund zitaweza kurejeshwa na kudumishwa. Tuna matatizo ya kijadi ya mashamba hasa sisi watu wa Pwani tunajua hilo. Katika BBI, imeweza tena kupeana fursa ya matatizo haya yaangaliwe upya. Kwa hivyo, itakuwa ni jambo la kushangaza na kuhuzunisha hususan kiongozi wa Pwani ikiwa atapinga ambapo anajua matatizo yeye mwenyewe ameyazungumzia na suluhisho likitaka kupatikana anarudi kupinga lile suluhisho ambalo lingepatikana. Hakuna matatizo ambayo tumesema eti kuna BBI tofauti tofauti. Niliposikia mara ya kwanza kwamba kaunti zingine zilipata BBI tofuati, nilidhani labda kuna moja inasema badala ya maeneo bunge 70 ambayo yaongezwe, moja inasema labda ni maeneo bunge 66 au 71. Nikifikiria kwamba katika pesa ambazo ziende kwa kaunti moja inasema asilimia 35 na nyingine inasema asilimia 40 lakini zote zinasema mambo ya kimsingi ambayo naamini wale walioweka sahihi ikiwemo mimi tuliweka tukijua kwamba tunataka pesa ziende mashinani na zote ambazo zinasemekana zinatofautiana bado zinazungumzia mambo ya asilimia 35, maeneo bunge 70 na mambo ya Equalisation Fund kama vile ambavyo tulikubaliana. Kwa hivyo, ikiwa mtu atapinga, pengine apinge na sababu zake lakini ukweli ni The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}