GET /api/v0.1/hansard/entries/1067994/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1067994,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1067994/?format=api",
"text_counter": 161,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Gertrude Mwanyanje",
"speaker": {
"id": 13245,
"legal_name": "Gertrude Mbeyu Mwanyanje",
"slug": "gertrude-mbeyu-mwanyanje"
},
"content": "Kama viongozi wa kike, kile kiti cha uwakilishi wa kike ndani ya Bunge kimetolewa lakini kimeenda pale Bunge la Seneti. Wamama 47 wakichaguliwa kwa kura ndani ya Seneti ni manufaa. Wataweza kupiga kura ndani ya Bunge la Seneti mbali na wale wa kuteuliwa. Hii ni manufaa kwetu. Nitazungumzia kuhusu maeneo Bunge 70 ambayo itaongezwa. Nataka kukuhakikishia ya kwamba sisi ambao hatutaweza kuendelea na uwakilishi wa kike ndani ya Bunge hili, tutarudi hapa tukiwa wawakilishi wa maeneo Bunge. Maeneo Bunge 70 yataleta uongozi na pesa mashinani kwa wananchi wetu."
}