GET /api/v0.1/hansard/entries/1067995/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1067995,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1067995/?format=api",
"text_counter": 162,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Gertrude Mwanyanje",
"speaker": {
"id": 13245,
"legal_name": "Gertrude Mbeyu Mwanyanje",
"slug": "gertrude-mbeyu-mwanyanje"
},
"content": "Tukipitisha Mswada huu, nakuhakikishia ya kwamba wanawake zaidi ya 40 kati ya zile nafasi 70 zimeongezwa, wataingia ndani ya Bunge hili. Hii itaondoa tashwishi ile tumepigana nayo ya Mswada wa kila wakati wa thuluthi mbili ambayo haitoshi ndani ya Bunge. Watu wa kutoka Pwani wanaunga mkono Mswada huu. Kama kuna Mbunge wa Pwani anapinga Mswada huu, ni kwa manufaa yake na pengine, njama fiche ambayo Wabunge wa Pwani hatuijui. Mambo ya ardhi yametajwa ndani ya Mswada huu. Dhuluma za mashamba kule kwetu zimetajwa pale ndani zipate suluhisho. Mambo ya uchumi wa samawati kule Pwani ina faida kubwa."
}