GET /api/v0.1/hansard/entries/1067996/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1067996,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1067996/?format=api",
"text_counter": 163,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kilifi CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Gertrude Mwanyanje",
"speaker": {
"id": 13245,
"legal_name": "Gertrude Mbeyu Mwanyanje",
"slug": "gertrude-mbeyu-mwanyanje"
},
"content": "Pesa ambazo zitapelekewa Wakilishi wa Wadi zitasaidia sana. Kuna Wakilishi wa Wadi ndani ya majimbo mengine ambao hawana pesa za maendeleo. Wakipata hizi pesa, gavana atakuwa na nyingi zaidi na wabunge wataongezeka. Hizi ni pesa za kusaidia mwananchi wa kawaida. Tuna hakika, tukifika kule mashinani, tutawambia watu wetu kuwa Mswada huu umekuja kwa ushirikiano wa kuungana mkono kwa Mhe. wetu Baba, Raila Amolo Odinga na mhe. Uhuru Kenyatta. Walizalisha mtoto huyu - BBI. Tuna imani ya kwamba tukipata zaidi maeneno Bunge 70, pesa za kusomesha watoto wetu na kujenga shule zetu zitaongezeka na Kenya itaendelea. Miradi mingi itafanywa. Tutapata faida zaidi, na hasa vizazi vyetu vijavyo."
}