GET /api/v0.1/hansard/entries/1068905/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1068905,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1068905/?format=api",
    "text_counter": 123,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Katika Kifungu cha kwanza cha Katiba yetu kinasema kwamba uwezo umepewa wananchi, na uwezo huo unafaa kutekelezwa kulingana na Katiba. Nguvu zote zimerejeshwa kwa wananchi, na nguvu zile zinafaa kutekelezwa kulingana na vile Katiba inavyoamrisha. Kifungu cha pili kinasema kuwa hakuna mtu wala taasisi yoyote ya Serikali inaweza kutekeleza jukumu lolote kama haijaruhusiwa na Katiba. Kwa hivyo, Katiba ndiyo mwanzo wa kila kitu katika sheria zetu. Kifungu cha 94 kinasema kuwa uwezo wa kutunga sheria umekabidhiwa Bunge. Hakuna taasisi isipokuwa Bunge inayo uwezo wa kutunga sheria ya kitaifa. Katika kutazama marekebisho haya, ni jukumu la Bunge kuangalia kwa undani kabisa, kwa sababu hatuwezi kupuuza kutelekeza jukumu letu."
}