GET /api/v0.1/hansard/entries/1068917/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1068917,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1068917/?format=api",
"text_counter": 135,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Sakaja",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13131,
"legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
"slug": "johnson-arthur-sakaja"
},
"content": "Bw. Spika, Bunge la Seneti liko na Kanuni na kuchanganywa sio hoja. Kanuni zetu zinasema wazi kwamba kama yule ambaye anazungumza amekiuka Kanuni za Seneti, yule ambaye anajaribu kumkosoa lazima aseme ni kipengee kipi ambacho amekiuka. Isiwe sababu haukubaliani na msimamo wa Seneta fulani, unaleta hoja la mjadala. Wiki iliyopita wakati nilikuwa ninatoa hoja zangu, karibu dakika 20 zilichukuliwa na watu ambao hawakubaliana na msimamo wangui. Sio eti nilikuwa nimekiuka Kanuni, lakini ni kwa sababu hawakua wanakubaliana na mjadala au maoni yangu. Bw. Spika, naomba kwamba ili Sen. Faki au yule mwingine atakaye kuwa anachangia aendelee na Mswada huu, badala ya kusimama kutoa hoja ya nidhamu kwa sababu hakubaliani naye. Wacha amalize, kisha utapata nafasi utoe maoni yako. Lakini hatua ya kusimama kila wakati kwa Hoja ya nidhamu kwa sababu hukubaliani na maoni ya mwenzako ni kinyume na sheria zetu kama Seneti."
}