GET /api/v0.1/hansard/entries/1068919/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1068919,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1068919/?format=api",
"text_counter": 137,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, nampongeza sana Sen. Sakaja kwa kusahihisha swala hilo. Nimetaja vifungu viwili vya Sheria ya Katiba ambavyo vinagongana. Ni ukweli, Bunge ndio taasisi inayojadili na kupitisha sheria katika Jamuhuri ya Kenya. Mswada wowote ambao unaletwa hapa Bunge ni lazima upitie hatua zote tatu kabla ya kupitishwa na kuwa sharia. Ni lazima usomwe mara ya kwanza, pili na tatu ambapo unaweza kupitishwa au ukataliwe. Ni nini majukumu ya Bunge katika vifungu hivi vitatu? Je, jukumu la Bunge ni kuangalia au kushangilia bila kutoa maoni yake? Je, Bunge ina jukumu ya kuweza kuchunguza Mwada wa sheria na kuona kwamba unaambatana na Katiba na sheria za kimataifa ambazo zinatumika katika nchi yetu? Kwa hivyo, hakuna kuchanganyika kokote hapo kama vile Seneta wa Nandi amesema. Nikizungumzia vipengee kadha wa kadha katika Mswada huu, kuna malengo mazuri. Je, tutayatekeleza malengo ambayo yanapedekezwa hapa? Kwa mfano, tunataka kujumuisha kila mtu katika nchi yetu? Lakini tukiangalia sheria zetu, hatujakuwa na ujumuishaji wa kila kabila katika Serikali ya nchi yetu. Vyeo vikubwa Serikalini vinalenga jamii moja. Tulikua Pwani juzi na Kamati ya Uwiyano ikiongozwa na Sen. Shiyonga ambapo tulikuwa tunaangazia swala la kuajiriwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kenya Maritime Authority (KMA). Tuliona pale kuwa ijapokua mkurugenzi yule hakuwa amehitimu kupata kazi ile, alipewa kazi hiyo kwa sababu wakubwa wake wote katika Wizara ya Usafiri wanatoka katika jamii moja na eneo moja. Bw. Spika, je, hili swala la inclusivity au kujumuisha kila mtu katika Kenya litaweza kutekelezwa kisawasawa? Kama sisi watu wa Pwani tutaweza kupewa nafasi moja ya Prime Minister au nafasi moja ya Deputy President? Hivi sasa inaonekana"
}