GET /api/v0.1/hansard/entries/1068921/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1068921,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1068921/?format=api",
    "text_counter": 139,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "tunabaguliwa wazi. Hata zile nafasi za kuteuliwa, kwa mfano katika Bunge, sisi kama watu wa Pwani hatuzipati. Jambo la pili ni kuwa hili swala la inclusivity lisiwe kwamba tunapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa; yaani, tupitishe halafu baadaye tunawachwa mataani kama tulivyo achwa muda uliopita. Jambo la tatu ni ofisi ya Ombudsman katika taasisi ya mahakama. Taasisi ya mahakama inatakikana iwe huru bila kuingiliwa na taasisi yote ama upande wowote katika maswala haya. Kuwepo kwa Ombudsman kwa hakika italeta mtafaruku katika taasisi ya mahakama, kwa sababu wakati Jaji atakapokuwa anaandika hukumu yake atakuwa anaangalia kwenye bega lake na kujiuliza, “Je, anaangaliwa na nani katika swala hili?” Mahakama itakosa uhuru na haki za kibinadamu zitaweza kudhulumiwa katika nchi yetu. Hatutakuwa na amani kwa sababu kila mtu atakuwa na shida ya haki hizi. Bw. Spika, hapo awali nafikiri ilikua 1982, kulikuwa na Mswada Bungeni wa kubadilisha Katiba. Kama sikukosea ilikua inataka kuondoa security of tenure ya majaji wa mahakama zote za Kenya. Wengi walioko katika Chama cha Mawakili wa Kenya walipinga swala hilo kwa sababu lilikuwa inapunguza uhuru wa majaji kusimamia swala hili. Mahakama ni taasisi ambayo inafaa iongozewe nguvu badala ya kupelekewa makachero au majasusi wakuweza kuchunguza majaji wanafanya nini. Bw. Spika, tatizo kubwa la mahakama hivi sasa ni kuwa wamepunguziwa ruzuku. Katiba ilikuwa imeweza kufikiria kuwa ili mahakama iwe huru na iamue haki kisawasawa, ni lazima iwe na fedha zake na uwezo wake wa kufanya kila jambo. Lakini kwa sasa, mahakama zetu zimefungwa na upande wa Executive. Hivi sasa ni kuwa mahakama hazina uhuru wa kutosha kuhakikisha kwamba wanatekeleza majukumu yao kisawasawa. Kwa sababu hiyo, swala kama hili la kuleta kachero ama Ombudsman kufanya uchunguzi katika mahakama, litaleta mtafaruku na kusababisha uhuru wa mahakama kupungua. Kuna mambo mazuri ambayo yamekuja katika marekebisho haya, kwa mfano, marekebisho ya kuweka Youth Fund. Hilo ni swala nzuri sana la kuhakikisha kuwa vijana wetu wanapata makazi na njia za kujikimu kimaisha bila ya kutegemea watu. Bw. Spika, swala ambalo litaleta utata ni uchaguzi wa Seneta mwanamke na Seneta mwanamume katika Bunge hili. Sisemi kuwa dada zetu Maseneta au Wabunge wanawake hawana majukumu ya kutekeleza. Wale Wabunge wanawake ambao wanahudumu katika Bunge la Kitaifa hivi sasa wanafanya kazi kubwa kule, ikilinganishwa na kuja hapa kupitisha tu maswala ya fedha na maswala mengine ambayo hayana uzito wa moja kwa moja kwa yule mwanamke na vijana walioko katika nchi yetu. Zile fedha ambazo wanapata viongozi wa kina mama katika Bunge la Kitaifa, zinasaidia pakubwa kutatua matatizo ya kielimu, kiuchumi na matatizo mengine ya huduma ambazo wananchi wanapata kwa sasa. Kwa hivyo, tukiwaondoa kule na tuwalete katika Bunge la Seneti, ndio tutajaribu kutekeleza usawa wa jinsia katika nchi yetu na Bunge letu, kwa hakika itakuwa hasara kubwa kwa vuguvugu la kuwapa nguvu akina mama."
}