GET /api/v0.1/hansard/entries/1068923/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1068923,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1068923/?format=api",
    "text_counter": 141,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, swala la maeneo Bunge limeleta utata kwa sababu halijatolewa kwa usawa. Tunaona kuwa maeneo mengi ambayo yanahitaji maeneo zaidi yamenyimwa. Ijapokua Mombasa inaongezewa viti vitatu vya Bunge, hiyo haitoshi kabisa. Mombasa imekuwa maradufu kwa muda wa miaka kumi na tunahitaji viti zaidi ya vitatu ambavyo tunaweza kupata hivi sasa. Pia tutakuwa tunakiuka Katiba kwa sababu swala la mipaka ya maeneo ya bunge hushughulikiwa na tume ya IEBC. Tume hii husimamia maswala ya ugavi wa maeneo bunge kwa kuzingatia wingi wa watu, mambo ya kiuchumi na usawa wa kuwakilishwa. Hii ni kwa sababu kuna maeneo mengi makubwa ambayo ni vigumu kuwakilishwa kikamilifu na mbunge mmoja. Kwa hivyo, nitaunga mkono marekebisho haya lakini hili swala la kuwa Mswada wa Kurekebisha Katiba ukishatoka kwa wananchi, usiweze kujadiliwa katika Bunge kwa sababu hili ni swala ambalo lazima tuliingilie kwa ndani hata kama itawezekana katika Mswada huu kulibatilisha lakini hii ifanywe na Bunge sababu Bunge hujadili Miswada mingi kabla hayajapitishwa na kuwa sheia. Hatuwezi kuwa sisi tumefungwa mikono wakati tunarekebisha sheria muhimu kama hii ya Katiba ya nchi. Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii."
}