GET /api/v0.1/hansard/entries/1068944/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1068944,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1068944/?format=api",
    "text_counter": 162,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Mbuga ya Wanyama ya Masaai Mara iliyoko katika Eneo Mbunge la Narok inafaidi wananchi kutokana na pesa nyingi tunayoita own source revenue . Kinyume ni kwamba kwetu hatupati faida hata kidogo bali maafa. Ninapoongea sasa hivi, kuna mtu atakayezikwa leo katika maeneo ya Bughuta katika Eneo Bunge la Voi. Mtu huyo aliuawa juzi na ndovu aliyemfuata mpaka shambani kwake. Mimea inaliwa na wanyama pori lakini kupata fidia imekuwa ngumu. Wakulima wale pia hawana pesa za kuweka uzio za umeme pia ni ngumu. Sehemu hizo zingetambulika kama sehemu maalum ya hifadhi ya wanyama pori au game reserves, tungeweza kujitengenezea uzio za umeme ili kuzia wanyama wa porini kuuwa binadamu, kuharibu mimea yetu au kuuwa wanyama wetu. Swala la pili ni faida kutokana na madini. Taita-Taveta ina madini mengi sana. Lakini hali ilivyo sasa, watu wanaofaidika na madini hayo ni watu wa nje. Wenyeji wa Taita-Taveta hawapati mrabaha kutoka kwa madini hayo. Wenyeji wa Kaunti ya Taita- Taveta hawapati miharaba zilizoangaziwa katika vipengee vya Mining Act, 2016 . Serikali ya Kitaifa haipatii watu wa Kaunti ya Taita-Taveta pesa zao ninazotokana na madini. Maswala haya ni lazima yaangaziwe katika BBI. Nilitarajia ripoti ya BBI ingeangazia swala la kwa nini wananchi wa Kenya, sana wenyeji wa Taita-Taveta. Wenyeji hawa hawana furaha kwa sababu wana rasilimali nyingi lakini hao ndio maskini zaidi katika nchi hii. Ningependa kusema kwamba kuna maswala fulani ambayo yaliangaziwa katika Mswada wa BBI ambayo yatatuhimiza kuunga mkono Mswada huu. Katika kutengeneza au kubadilisha katiba hauwezi kuwafurahisha wananchi wote. Kuna mengi yatakayo furahisha wananchi na mengi yatakayowakera baadhi ya wananchi. Yanayo tufurahisha katika Mswada huu wa BBI, ni kuongezwa kwa idadi ya maeneo bunge. Kaunti ya Taita- Taveta ina wapiga kura zaidi ya 200,000 ilhali ina maeneo bunge manne. Mswada huu wa BBI usipopita, maeneo bunge katika Kaunti ya Taita-Taveta yatapungua ili tubaki na maeneo bunge mawili au matatu. Kwa mfano, eneo bunge moja likipotea, Kaunti ya Taita Taveta itapata hasara ya Kshs140 milioni. Tukipoteza maeneo bunge mawili, tutakuwa tunapoteza zaidi ya Kshs280 milioni. Kaunti ya Taita-Taveta inafurahia Mswada huu wa BBI kwani unapendekeza kubakisha maeneo bunge manne yalioko sasa. Pili, Mswada huu wa BBI unaimarisha ugatuzi kwa kupendekeza rasilimali zaidi kuendea serikali za ugatuzi. Katiba ya 2010 lilipendekeza asilimia 15 ya upato wa nchi kuendea serikali za ugatuzi. Mswada wa BBI unapendekeza asili mia 35 ya upato. Wale wanaopiga Mswada huu wa BBI wanasema kwamba ikiwa kufikia sasa Serikali ya Kitaifa haijaweza kupeleka asilimia 15 ya upato wa nchi katika serikali za ugatuzi, je wataweza aje kupeleka asilimia 35? Mwaka jana tulipokuwa na mjadala mkali kuhusu ugavi wa rasilimali, tulikuwa tunapigani pesa ziongezwe kutoka Kshs316.5 bilioni mpaka Kshs370 bilioni. Ninafuraha kwamba tulifaulu kuhimiza Serikali ya Kitaifa kupeleka rasimali zaidi katika serikali zetu za ugatuzi. Hivi sasa, kuna pesa nyingi sana ambazo zinabaki katika Serikali ya Kitaifa ambayo ingefaidi sana serikali za ugatuzi. Kwa mfano, pesa zinasoendea mashirika kama"
}