GET /api/v0.1/hansard/entries/1068948/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1068948,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1068948/?format=api",
"text_counter": 166,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Swala la ugatuzi ni swala nzito sana kwangu kama Seneta wa Kaunti ya Taita- Taveta. Wananchi wetu wanfaidika sana na maendeleo kutokana na ugatuzi. Kaunti ya Taita-Taveta ni moja wapo ya kaunti ndogo nchini na wengi wanaopinga ugatuzi uuliza inakura ngapi? Kwa kweli, kura zetu ni chache sana. Sisi mfumo huu wa ugatuzi ni baraka kubwa sana kwetu. Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa ugatuzi, Kaunti ya Taita- Taveta imepokea zaidi ya Kshs4.5 bilioni za maendeleo kila mwaka. Kabla ya mfumo wa ugatuzi, haikuwa inapata kiwango hicho cha pesa. Tunapata pesa nyingi sana za maendeleo katika mfumo huu wa ugatuzi."
}