GET /api/v0.1/hansard/entries/1068949/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1068949,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1068949/?format=api",
    "text_counter": 167,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Kuanzia mwaka 2013, mfumo wa ugatuzi ulipoanza, hakuna mradi umefanywa katika Kaunti ya Taita-Taveta kutokana na pesa za Serikali ya Kitaifa unaozidi Kshs200 milioni. Pesa zaidi tulipata kwa mradi mmoja haukuzidi Kshs50 milioni. Hata hivyo, mwaka huu, Kaunti ya Taita-Taveta ilipata msaada kutoka kwa Benki ya Dunia wa Kshs900 milioni ya mradi wa maji. Mwaka wa 2018, niliuliza swali hapa Bungeni nikitaka Wizara ya Maji itueleze miradi yote nchini katika wizara hiyo. Ripoti hiyo ilipoletwa hapa Bungeni, nilishangaa kuona Kaunti ya Embu ilipata kiasi cha Kshs2.5 bilioni za miradi ya maji kuanzia 2013 hadi 2018. Kaunti ya Murang’a ilipata kiasi cha Kshs6 bilioni, Kaunti ya Elgeyo-Marakwet ilipata kiasi cha Kshs25 bilioni kupitia miradi ya mabwawa za Arror and Kimwarer. Kaunti ya Kwale ilipata Kshs10 bilioni kupitia mradi wa bwawa la Mwate. Kaunti ya Makueni ilipata kiasi cha Kshs35 bilioni kupitia mradi wa bwawa la Thwake. Ingawa kuanzi mwaka wa 2013 hadi 2018, Kaunti la Taita- Taveta haikupata miradi yoyote ya maji. Kwa hiyo, tunapigania ugatuzi kwa sababu maendeleo yetu mengi yanatokana na ugatuzi."
}