GET /api/v0.1/hansard/entries/1068957/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1068957,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1068957/?format=api",
    "text_counter": 175,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Yale masuala ambayo labda hayako vizuri katika serikali yetu wakati huu ni kwamba ugatuzi ni jambo nzuri lakini kutoa pesa kuzipeleka kwa kaunti ili zifanye maendeleo kumekuwa kizungumkuti. Nina imani kwamba tukiwa na uongozi mzuri unaoangalia mambo ya fedha na kumaliza ufisadi, tutakusanya fedha za kutosha na kwa wakati unaofaa ili ziende katika kaunti kufanya maendeleo. Mambo ya ufisadi yanaua maendeleo katika nchi yetu tukufu ya Kenya. Leo tunaambiwa kuwa billioni mbili fedha za Kenya zinapotea kila siku. Tukifunga huo mfereji wa ufisadi, basi zile pesa za kwenda kufanya maendeo mashinani zitapatikana na tutazidi kudumisha ugatuzi. Mambo wakati huu yamekuwa magumu zaidi kwa sababu ya janga la Korona. Shirika la Ukusanyaji Ushuru (KRA) halikusanyi ushuru inavyopaswa lakini janga hili litaenda kuwa nasi. Hatutakaa nalo milele. Kuna watu wanaouliza kama wakati huu wa janga la korona ni wakati mzuri wa kubadilisha katiba. Mchakato huu wa kubadilisha katiba ulianza kabla ya janga hili kuja. Je, tukisema hatutabadilisha Katiba wakati huu na mazuri yote yaliyomo kwenye Mswada wa Marekebisho ya Katiba, 2020, kuna mkataba gani na janga hili? Litaisha"
}