GET /api/v0.1/hansard/entries/1068959/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1068959,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1068959/?format=api",
    "text_counter": 177,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "lini? Hatujui. Hatujui kama litakuwa kama mafua au kohozi ambalo tunaendelea nalo milele na milele. Mambo ya kusema tusibadilishe Katiba kwa sababu kuna Korona hayana umuhimu wowote kwa sababu hatujui kama janga hili litaenda mpaka lini. Mambo ya kukopa sana ili kufanya maendeleo yanatufisha moyo sana hapa Kenya. Kabla ya mwaka wa 2012 tuliweza kumudu asilimia 95 ya bajeti yetu. Mwaka wa 2012 asilimia 95 ya bajeti ya Kenya ilichangiwa na fedha zilizotoka Kenya kwenyewe. La kuvunja moyo sasa ni kwamba bajeti yetu ni Kshs3 trillioni katika nchi inayokusanya chini ya Kshs2 trillioni. Jambo hili linaonyesha kuwa katika mwaka wa Kifedha wa 2021/2022 bado tutaingia katika bonde la kukopa zaidi ya Kshs1.6 trillioni. Kwa nini tusiiishi kadiri ya mapato yetu? Kwa nini tunaishi na madeni? Tuna madeni na tunaendelea kuingia kwa mengine na tutaendelea kuingia kwa mengine zaidi. Tunaongea mambo ya ugatuzi – ambao ni mzuri- lakini kama tutakuwa tukitumia fedha zote kulipia madeni ambayo hatafanya maendeleo kwa maeneo fulani pekee. Maeneo kama Taita Taveta hayapati miradi hiyo lakini ikifikia wakati wa kulipa tunalipa sote. Jambo hill la good financial management na debt management strategy lazima tuliangazie, tuache kukopa na tuishi within our means. La mwisho ni kwamba watu wanauliza kama kuubadilisha Mswada huu. Hatuwezi kwa sababu unatoka kwa wananchi na umepitia kwa county assemblies na hawakuubadilisha. Kama county assemblies zote zingeamua kubadilisha, tungekuwa na Miswada mingapi inayokuja kwa Seneti na Bunge la Kitaifa. Tayari National Assembly wamepitisha Mswada huu bila kuubadilisha. Je, sisi kama Seneti tukiamua kuubadilisha, ni upi utakaoenda katika referendum ? Naomba tuheshimu wananchi wetu. Tuuptitishe vile ulivyo kama ulivyotoka kwa wananchi, ukaenda county assemblies na National Assembly kwa sababu itazuia mkanganyiko kuhusu Mswada utakaoenda katika kura ya maoni. Mswada huu hata tukiungusha leo, lazima uende kwa kura ya maoni. Kuna mambo mawili yanayofanya Mswada uende kwa kura ya maoni. La kwanza ni kama mwananchi ameamua kubadilisha Katiba na yale masuala anayoangazia ni yale ambayo hayajaangaziwa katika Ibara ya 255 ambayo ni Structure of Governance na vile Bunge linavofanya kazi. Hayo ni masuala ambayo hayahitaji kwenda katika kura ya maoni lakini yanaweza kutengenezwa na Bunge. Ukienda Bungeni na Bunge iamue kuupitisha, basi ule Mswada utaenda kwa Rais na kuidhinishwa. Bunge likiletewa Mswada kuhusu mambo ambayo hayajaangaziwa katika Ibara 255 halafu iamue kuuangusha Mswada ule, ni lazima uende kwa kura ya maoni na wananchi waamue wenyewe. Mswada mwingine ambao ni lazima uende kwa kura ya maoni ni ule ulioangazia masuala mengine yaliyo katika Ibara 255 ambayo ni Structure of Governance, working ofParliament na How to Change the Constitution . Mswada huo ukija Bungeni ni lazima uende kwa kura ya maoni hata tukiuangusha ama kuupitisha. Huu wa leo tukiupitisha au kuuangusha ni lazima uende kwa kura ya maoni. Mh. Spika, ninashukuru kwa nafasi uliyonipa ili kuangazia masuala ya Mswada huu wa BBI. Ninajua BBI itaenda kubadilisha maisha ya mwananchi wa Kenya."
}