GET /api/v0.1/hansard/entries/1068979/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1068979,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1068979/?format=api",
    "text_counter": 197,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Zawadi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13176,
        "legal_name": "Christine Zawadi Gona",
        "slug": "christine-zawadi-gona"
    },
    "content": "zote za Kaunti ya Kilifi. Katika matembezi hayo, niliona jinsi hospitali zetu zilikuwa vibaya. Baada ya pesa kuteremshwa mashinani, nimenona hizo hospitali zimetengenezwa, isipokuwa tunakosa madawa na wauguzi kwa sababu pesa ni chache. Ndio maana ninakubali kwamba endapo marekebisho haya ya Katiba yatapitshwa, ninaamini wauguzi wataajiriwa na madawa kupatikana hospitalini. Hilo ndio tatizo kubwa mashinani. Bw. Spika, pia nilikuwa katika Kamati ya Elimu na nikagundua watoto wengi hawaendi shule wakiwa wadogo. Wengi wao walichelewa kuanza shule hadi wafike labda umri wa miaka 10 au zaidi. Ni katika umri huo ndio wangeweza kumudu kutembea hadi shule kwa sababu shule zenyewe zilikuwa mbali sana na pia chache. Watoto wa chekechea walilazimika hadi waweze kutembea aidha kilo mita 10 au zaidi ili kufika shuleni. Baada ya kupitisha Katiba, shule za chekechea zimejengwa nyingi mashinani. Lakini hizo shule zinakosa walimu kwa sababu ya uhaba wa pesa. Kwa hiyo, ninaunga mkono mapendekezo ya marekebisho ya Katiba. Endapo itapita, basi pesa zikifika mashinani, ninaamini walimu wengi wa chekechea wataajiriwa. Ninakubalina na wenzangu wengi walioulizwa kwa nini marekebisho yaja saa hii na sio mwanzoni. Niliwasikiliza na sasa ninakosoa. Wengi walisema kuna mambo kama vile korona ambayo yangeletwa Bungeni. Sikumbuki kukiletwa Mswada hapa kuhusu korona na ukakosa kujadiliwa kwa sababu ya kuja kwa Mswada wa mapendekezo ya marekebisho ya Katiba. Hakuna aliyeleta Mswada wake na ukakosa kujadiliwa."
}