GET /api/v0.1/hansard/entries/1068981/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1068981,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1068981/?format=api",
    "text_counter": 199,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Zawadi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13176,
        "legal_name": "Christine Zawadi Gona",
        "slug": "christine-zawadi-gona"
    },
    "content": "Bw. Spika, ninakubaliana na wenzangu kwamba ni kweli mwanamke ndiye anawajibika. Fanya hesabu haraka tu uangalie hapa ndani kumesalia wanawake wangapi na wananume ni wangapi. Kisha fanya hesabu uone wanaume na wanawake huwa wangapi katika Bunge hili la Seneti. Utakuta mwanamke anawajibika na ndio maana wengi wako hapa ndani wanasikiza jinsi Mswada huu unavyoendelea. Hivyo basi, ninakubali mwanamke mmoja awe katika Bunge la Seneti. Vile vile, ningetamani mwanamke mwengine abakie kwenye Bunge la Taifa. Hii ni kwa sababu, kuna changizo kubwa mwanamke angefanya akiwa kule. Kwa hivyo, nakubaliana kwamba kungekuwa na mwanamke katika Bunge la Taifa na Seneti."
}