GET /api/v0.1/hansard/entries/1068986/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1068986,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1068986/?format=api",
"text_counter": 204,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Zawadi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Vile vile, nashukuru na niseme kwamba angalau watu wa Kilifi tumeweza kuwa na barabara mbili au tatu. Sisi pia tunajiita Wakenya. Pale nyuma, tulikuwa tukisema pwani si Kenya. Hii ni kwa sababu hatukuwa tunayapata mengi. Angalau kuna kidogo tunaweza hesabu. Kwa mfano, barabara. Sio nyingi, lakini zipo. Sio kama vile ilivyokuwa mwanzoni, wakati tulikuwa hatuna kabisa. Nakubaliana kwamba, iwapi pesa zitakuwa mashinani, hatutakuwa tunatengemea Bunge la Taifa au Serikali kuu itutengenezee barabara. Tutakuwa na uwezo huo kama kaunti wa kutengeneza barabara na vitu vingine vingi ambavyo vinakosekana. Kama barabara ni ya murram, sio lazima Executive ikubali ndiposa ifanyike. Itakuwa inafanyika."
}