GET /api/v0.1/hansard/entries/1068989/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1068989,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1068989/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Zawadi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Iwapo itapita, wale wabunge ambao watabahatika kuchaguliwa, tutapata waziri wetu kutoka kwa wale wabunge. Mimi naunga mkono. Hii ni kwa sababu, ni mara ngapi tuliita Waziri wa Kilimo hasa wakati ule wa nzige? Tulisumbuka sana kuita Waziri wa Kilimo na Ilikuwa vigumu sana kupatikana. Vile vile, tumemwita Waziri wa Barabara mara nyingi lakini inakuwa shida kupatikana. Kwa nini? Ndio maana naunga mkono Katiba hii au mapendekezo haya. Iwapo itapita, basi waziri watatoka hapa, haina haja tukawafuate mbali. Tukimtaka, tutampata hapa hapa, kwa maana ni mmoja wetu, tuko naye, and twala naye. Ni haraka sana kuonana naye na kutatua mambo ambayo tutakuwa tuko nayo. Sasa hivi, tukiwataka, kuwapata ni kama mbingu na nchi. Hawapatikani. Tunawatafuta hadi kuchoka. Lazima wawe summoned ndio aweze kupatikana."
}