GET /api/v0.1/hansard/entries/1069698/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1069698,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1069698/?format=api",
"text_counter": 439,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Zawadi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Ingawa kuna kaunti nyingi ambazo hazitapata maeneo bunge zaidi, ningependa kuwakumbusha kwamba kila kilocho na mwanzo hakikosi mwisho. Sio kwamba tunawaonea au hatuwapendi, lakini siku haikuwa yao. Wakati utafika siku moja na watapata maeneo bunge mengine. Na hata kama hawatapata sehemu zaidi za uwakilishi Bungeni, nina hakika kuna mengine ambayo wameyapata mazuri kulingana na hiyo BBI. Ukiiangalia viziri utakuta hapo ndani kuna mambo mazuri mengi na mabaya hayakosi kwa sababu ni mwanadamu aliyeitengeneza. Ninaamini tulivyoanza kwa mwendo huu, tumeanza safari na nina hakika ina mwisho mwema."
}