GET /api/v0.1/hansard/entries/1069744/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1069744,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1069744/?format=api",
"text_counter": 485,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mutula Kilonzo Jnr",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13156,
"legal_name": "Mutula Kilonzo Jnr",
"slug": "mutula-kilonzo-jnr"
},
"content": ".: Hoja ya nidhamu, Bi. Naibu Spika. Ninamuomba Kiongozi wa Walio Wengi atusikize kwa makini. Hili sio jambo la kupuuza. Ninaomba iwapo ingewezekana Hoja hii ingechapishwa kwa Kiswahili katika Orodha ya Shughuli za Bunge. Kisha, Kiongozi wa Wengi pamoja na yule atakayemuunga mkono, waendeleze Hoja hii kwa Kiswahili. Rais Suluhu alisema anafurahia Kiswahili chetu kwa sababu kiko na ucheshi. Kwa hivyo, ni wakati wetu na jukumu letu pia tujadiliane Hoja hii kwa Kiswahili. Nakala niliyonayo hapa imeandikwa kwa Kiswahili. Ninashangaa kwa nini Kiongozi wetu anaanza kwa Kingereza ilhali nakala ambayo anataka tuunge mkono imeandikwa kwa Kiswahili. Je, huu ni ungwana?"
}