GET /api/v0.1/hansard/entries/1069754/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1069754,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1069754/?format=api",
    "text_counter": 495,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Shukran, Bi. Naibu Spika. Kwanza, natoa shukran kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan. Tuna mshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia kwa sababu tunawazia jambo muhimu ambalo alileta. Kitu cha kwanza, tunawapa kongole watu wa Tanzania kwa sababu katika historia ya nchi hiyo, kutoka wapate uhuru mpaka sasa, ni Rais wa kwanza mwanamke katika Muungano wa Mashariki ya Kati. Bi. Naibu Spika, sisi kama watu wanaotoka sehemu ya Pwani tunajua kuzungumza Kiswahili. Lakini, Rais wa Muungano wa Jamhuri ya Tanzania aliweza kuongea Kiswahili safi. Nilipokisikiliza, nilisema hata kama tunatoka maeneo ya Mombasa, Kilifi ama Malindi hatuongei Kiswahili kama hicho. Kiswahili chake kilikuwa safi kabisa."
}