GET /api/v0.1/hansard/entries/1069758/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1069758,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1069758/?format=api",
    "text_counter": 499,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Bi. Naibu Spika, tumeona katika mipaka hiyo kuwa sio wanyama pekee yake. Katika maeneo tofauti ya mipaka kuna jamaa ambao wanaishi pamoja. Tukiangalia upande kama Pwani, ukitaka kwenda Tanga ama Dar es Salaam unaweza kupitia maeneo ya Horohoro ama Lungalunga. Hiyo ni mipaka ambayo jamaa wa Kidigo katika Jamii ya Mijikenda wanaishi, humu nchini na vile vile upande wa Tanzania kupitia sehemu za Tanga na Dar es Salaam. Ikiwa wanyama wanashirikiana na binadamu kuketi pamoja, biashara zetu pia zinaweza kuwa pamoja. Tukija katikati tuko na eneo ambalo liko na Wataita na Taveta, ambao wako Voi na ni wengi. Nao pia wanaushirikiano katika mpaka huo."
}