GET /api/v0.1/hansard/entries/1069761/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1069761,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1069761/?format=api",
    "text_counter": 502,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Vile vile, tuko na eneo la Namanga. Ukitoka hapa Nairobi utapita eneo la Namanga. Kule kuna Wamaasai. Bi. Spika wa Muda, nakusifu kwa sababu wewe ni mmoja wao. Ikiwa mnaishi kwa amani upande wa Namanga Kenya na upande ule mwingine. Hatuwezi kujua tofauti kwa sababu majina yanafanana. Vile mnaishi na tabia zinafanana. Ukienda upande wa Namanga kule Tanzania, Wamaasai wanaoishi kama ndugu. Kwa hivyo, ni jambo ya kufurahisha ikiwa Rais wa Tanzania anaweza kuja hapa na kutueleza kwamba wanyama wanashirikiana, binadamu wanashirikiana na mipaka iko pamoja. Sisi tunaishi kama ndugu na hatuwezi kugeuza Maisha kwanzia sasa na milele. La muhimu katika ushirikiano huo, alisema ya kwamba ingekuwa bora tukiongeza biashara pande zote mbili. Tusilemeane kwamba wengine wanaleta nyingi zaidi ya wengine. Tuone kwamba tutakuwa na ushirikiano bora."
}