GET /api/v0.1/hansard/entries/1069762/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1069762,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1069762/?format=api",
"text_counter": 503,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, katika Hotuba yake, alisifu Bunge la Seneti na Bunge la Kitaifa akisema kwamba ni jambo bora aliyoiona. Ni kwamba tunaongea Kiswahili ambacho ni cha kufurahisha sana. Kama alivyokuwa akisema Kiogozi wa Walio Wengi, alijaribu kuongea lakini katikati akageuza; ni kama maji yalizidi unga. Akasema kwamba angependelea kuongea kwa lugha ya Kiingereza, lakini hiyo ni mojawapo ya tafakari zetu. Kiongozi wa Walio wa Wengi amejaribu sana. Ni mara yangu ya kwanza kusikia akiongea Kiswahili. Ni kizuri lakini labda alikuwa na hofu ya kukosea. Nina matumaini makubwa ya kwamba kwa vile sasa tuko na ile Hotuba yake katika lugha ya Kiswahili, Wenzetu maseneta watakaopata nafasi ya kujadili Hotuba ile wataongea kwa lugha ya Kiswahili."
}