GET /api/v0.1/hansard/entries/1069766/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1069766,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1069766/?format=api",
    "text_counter": 507,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Mwisho ni kumsifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aligusa jambo la janga hili la COVID-19. Alisema kuwa sisi kama majirani tunaoishi na kufanya biashara pamoja, tunashirikiana kwa mambo mengi. Ikiwa ushirikiano huo utaendelea, ni vizuri kulipiga vita janga hili pamoja. Kenya imeendelea mbele zaidi kupiga vita hili janga ya COVID-19, lakini upande wa Tanzania, kidogo walienda pole pole. Jukumu letu ni kutia maanani Hotuba ya Rais ya kwamba wamekubaliana kuanzisha--- Nilifurahi sana nilipoana kwamba wote waliokuja katika ziara hii na kuingia Bungeni kusikiza Hotuba ya Rais walikuwa wamevaa barakoa wote. Hiyo ni ishara kuwa wao pia wana juhudi na mwelekeo wa kupambana na hili janga ambalo linaweza kutumaliza sote. Watu wanaosikizana, kufanya biashara pamoja, kulala katika hoteli moja na kukula katika chumba cha malaji pamoja, ikiwa hawatavaa barakoa inaweza kuwa hatari, iwe ni upande wa Kenya ama Tanzania."
}