GET /api/v0.1/hansard/entries/1069776/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1069776,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1069776/?format=api",
    "text_counter": 517,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mutula Kilonzo Jnr.",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13156,
        "legal_name": "Mutula Kilonzo Jnr",
        "slug": "mutula-kilonzo-jnr"
    },
    "content": "Asante, Bi Spika wa Muda. Kwanza ninamshukuru Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa Hotuba yake ambayo imeleta maridhiano. Kwa jamii ya Watanzania ndugu zetu tukubalie tuendelee kuwapatia risala zetu za rambi rambi kwa kumpoteza kiongozi wao, Rais John Pombe Magufuli. Mungu amrehemu na amlaze mahali pema peponi. Jambo ambalo Rais wa Tanzania alifanya au Hotuba ambayo alitoa imekomboa mambo ambayo yamewashinda wanaume. Viongozi wanaume wameshindwa kuleta uwiano katika Afrika Mashariki. Imebidi mwanamke awaonyeshe viongozi wanaume njia. Jambo hili ni la muhimu. Wale ambao kama sisi tunapigia debe Mswada kama ule ambao tumepitisha leo. Ni kwa sababu katika maoni yangu, viongozi ambao watachaguliwa katika kaunti zetu 47 ni wanawake. Ni njia mufti kutafuta uongozi wa kitaifa kupitia kwa Bunge hili. Jambo la kuwezesha wanawake hao wapate nafasi kama hiyo ni kuchaguliwa katika kaunti zetu. Kuna jambo lingine. Kuna watu hawakumbuki historia yetu na ni vizuri niseme. Ni kwa sababu Sen. Wako na marehemu mzee wangu, Baba, Sen. Mutula Kilonzo, walisomea Dar es Salaam wakati ambapo hakukuwa na shahada ya uanasheria katika vyuo vyetu huku Kenya. Walifunzwa sheria na wengine wengi ambao ni majaji. Wengine kama mwenyekiti wa timu ya Gor Mahia, Ambrose Rachier, walisomea uanasheria nchini Tanzania. Bi. Spika wa Muda, lakini mambo ambayo yanazungumziwa hapa ni nafasi za kibiashara kwetu sisi Wakenya. Kuna nafasi za kibiashara za Watanzania. Ni jambo la muhimu. Kwa sababu wale ambao ni wafanyibiashara na wengine ambao ni wateja wetu katika kazi zetu mbali mbali wametuambia kwamba wamepata shida. Mahindi ambayo yanatoka Tanzania yanapitia kwako Namanga, Bi Spika wa Muda. Yale mengine yanapitia Emali na Kibwezi. Yanaletwa Kenya kwa bei nafuu. Lakini mahindi ambayo tunayapanda Kenya hayawezi kuuzwa Tanzania. Kwa muda mrefu ilikuwa ni vigumu sana kuuza maziwa Tanzania. Nakumbuka nikiwa katika nchi ya Zambia, yule ambaye ni msimamizi wetu huko kama balozi aliniambia kwamba njia mufti ya sisi kuingia katika Jumuiya ya Southern African Development Community (SADC), ambayo Tanzania ni mwanachama, ni kupitia Tanzania. Bi. Spika wa Muda, kwa hivyo, tunataka kumshukuru kwa dhati Rais wa Tanzania kwa mambo na matamshi na kufunguliwa njia kwa biashara ya Wakenya na Watanzania ili Wakenya na Watanzania tutafute njia na kutafuta pia Waganda. Tunataka Rais Uhuru Kenyatta, Rais Suluhu Hassan na Rais Museveni wakutane na Rais Kagame pia ili tutafute njia ambayo tunaweza kufanya Jumuiya hii idumishwe."
}