GET /api/v0.1/hansard/entries/1069778/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1069778,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1069778/?format=api",
    "text_counter": 519,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mutula Kilonzo Jnr.",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13156,
        "legal_name": "Mutula Kilonzo Jnr",
        "slug": "mutula-kilonzo-jnr"
    },
    "content": "Tunataka tuwe na kampuni moja ya ndege kama vile tulikuwa na kampuni moja ya ndege zamani. Pia, tunaweza kuwa na kampuni ya reli na kampuni za vitu vingi hata mawasiliano kama ilivyokuwa kabla ya Jumuiya hii kuvunjiliwa mbali mwaka wa 1977. Je, ni kwa nini? Ndio kwa sababu tunasema uongozi umelegea. Tungekuwa na mtu kama Rais Suluhu kabla hatujafanya mkataba wa ujenzi wa reli tulioufanya na Wachina, ambayo inapitia kwako, ingekuwa rahisi. Deni hili ambalo tuko nalo na hawa Wachina halingekuwepo. Bi Spika wa Muda, hivi maajuzi nilitembelea nchi ya Dubai. Nimesikia kwamba wamefungua bandari yao Tanzania ili wafanye biashara kwa njia rahisi kuliko Bandari ya Mombasa. Ninauliza swali hili na hawa wenzetu Maseneta kutoka Pwani watajibu haya maswali."
}