GET /api/v0.1/hansard/entries/1069779/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1069779,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1069779/?format=api",
"text_counter": 520,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mutula Kilonzo Jnr.",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13156,
"legal_name": "Mutula Kilonzo Jnr",
"slug": "mutula-kilonzo-jnr"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, bandari yetu kuna dock au kizimbani . Kuna mfanyibiashara mashuhuri ambaye amekomboa sehemu ya kufanyia biashara. Sisi Wakenya tumeshindwa kutafuta mtu ambaye tunaweza kuungana naye ili tufanye public privatepartnership katika bandari ya Mombasa ili tuimarishe huduma. Wafanyibiashara wengi wanahamia Rwanda au Tanzania. Ni lazima tujiulize ni kwa nini wanafanya hivyo. Mimi hupenda sana kuwaona wanyama wa porini. Kuna wakati nilienda pamoja na familia yangu Tanzania kuwaona wanyama. Tulienda Manyara, Ngorongoro, Kirawira na Mbuga ya Wanyama ya Serengeti. Nilishangaa kuona sehemu ambazo mbuga za wanyama zimetengewa ili kudumisha sekta ya utalii. Bei za hoteli za Kirawira, Serengeti, Ngorongoro na Manyara ni ghali mara tatu kuliko za Mombasa na Nairobi. Jambo la kushangaza ni kwamba hoteli zote zilikuwa zimejaa watalalii. Ni kwa nini? Kuna watalii wanaokuja kusheherekea sikukuu ya Ramadhan na wanapitia Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Utapata gari za Tanzania hapo, lakini hakuna gari za Wakenya utaziona uwanja wa ndege wa Tanzania."
}