GET /api/v0.1/hansard/entries/1069780/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1069780,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1069780/?format=api",
"text_counter": 521,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mutula Kilonzo Jnr.",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13156,
"legal_name": "Mutula Kilonzo Jnr",
"slug": "mutula-kilonzo-jnr"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, mimi ninaona kama ni malaika ametumwa ili tufanye hii kazi. Nimetumia barabara aliyozungumzia inayotoka Voi hadi Mwatate. Hiyo barabara ilikuwa mbovu sana na kuna sehemu za utalii za kifahari. Wale ambao hamjatembea sehemu hiyo kuna hoteli maarufu inayoitwa Salt Lick Safari Lodge. Kuna mahali pa kifahari ambapo hema hutengenezwa huko Mwatate. Mnaweza kutembelea sehemu hiyo ukielekea Tanzania wakati barabara hiyo itakamilishwa. Waheshimiwa maraisi hawa wawili wamesema watajenga barabara hiyo ili kuimarisha mawasiliano kati ya wananchi wa mataifa haya mawili. Kutoka Arusha hadi Manyara ni karibu kilomita 500 au 600. Hakuna babarabara yoyote kama hiyo nchini Kenya. Nilistaajabu wakati Rais Magufuli alipata uongozi. Badala ya kuwa na sherehe kubwa ambayo ingeharimu Serikali ya Tanzania pesa nyingi kwa kuandaa karamu ya ushindi wake, walitengeneza barabara ambayo inatumiwa na wazima moto na wanaosafirisha wagonjwa hospitali. Gari zinapita katikati. Kenya inajenga barabara za ghorofa eneo la Mombasa Road kutoka Mlolongo. Hakuna mtu ambaye anafikiria ni kwa nini hatuwezi kuwa na barabara inayoweza kuwafikisha wagonjwa au wazima moto kwa haraka. Kuna ripoti kwamba wakati barabara ya Thika ilifungwa hivi majuzi, kuna mtoto alikufa. Hii ni kwa sababu barabara ilifungwa na hakuna mahali ambapo wazazi wake wangeweza kupitia ili wafike hospitali kwa haraka."
}