GET /api/v0.1/hansard/entries/1069785/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1069785,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1069785/?format=api",
"text_counter": 526,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mutula Kilonzo Jnr.",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13156,
"legal_name": "Mutula Kilonzo Jnr",
"slug": "mutula-kilonzo-jnr"
},
"content": "Wakati Seneta Wako atapewa nafasi kuzungumza, labda atatueleza jambo hili lilitoka wapi. Nilimwuliza dereva aliyekuwa ananielekeza pamoja na familia yangu jina lake. Unajua sisi tuna tabia ya kuuliza watu majina yao. Aliniambia anaitwa Amos. Mimi sikuridhika na jina Amos. Nilitaka aniambie jina lake la pili ili nijue ni wa kabila ipi. Ukabila wetu na mambo ambayo tunafanya ni tabia mbaya. Tunauliza maswali hayo ili tujue kama tunaweza kunong’onezana kwa lugha ya mama. Bi. Spika wa Muda, kuna kamati kubwa ambayo ina wanachama wanne wanaotoka kabila moja. Wakati mkutano unaendelea, wanazungumza kwa lugha ya mama. Ni kwa nini? Nilimwuliza huyo dereva, “Wewe unaitwa nani?” Alinipa jina la kwanza. Nilimwuliza jina la pili, akasema kuwa huwa hawasemi jina la pili huko Tanzania. Nilimwuliza kwa nini, akaniambia kuwa hawana ukabila kama sisi Wakenya. Tanzania ina makabila zaidi ya mia moja. Hata kama tumepitisha Mswada tuliyoujadili leo, tunaka tuwe na nchi ambayo ukisema jina lako ni Gertrude, Amos ama Stewart, yatosha, na hakuna atakayekuuliza umetoka wapi."
}