GET /api/v0.1/hansard/entries/1069786/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1069786,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1069786/?format=api",
"text_counter": 527,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mutula Kilonzo Jnr.",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13156,
"legal_name": "Mutula Kilonzo Jnr",
"slug": "mutula-kilonzo-jnr"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, kuna stakabadhi za Serikali ambazo zinahijataji useme wewe ni wa kabila lipi. Wewe ni wakili kama mimi. Ukienda kortini utaona kuwa kuna stakabadhi, kwa mfano, charge sheet unahitajika kuandika kabila lako. Wakati utafika tuseme kwamba jambo hili halileti utengamano na uwiano katika jamii zetu. Iwe ni hatia kuzungumza lugha ya mama kwenye mkutano au hadharani. Ukitaka kuzungumza lugha ya mama, ujifungie uzungumze kwako nyumbani ukiwa peka yako kwa sababu unaweza kuwa umemwoa mtu ambaye si wa kabila lako. Hilo ni jambo ambalo tunafaa kuiga kutoka kwa Watanzania. Tungepatiwa nafasi, tungehamia huko tutafute familia, lakini kwa sababu tumezaliwa huku, tutakaa lakini lazima tuige mfano wa Watanzania."
}