GET /api/v0.1/hansard/entries/1069974/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1069974,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1069974/?format=api",
    "text_counter": 164,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi South, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Ken Chonga",
    "speaker": {
        "id": 13374,
        "legal_name": "Richard Ken Chonga Kiti",
        "slug": "richard-ken-chonga-kiti"
    },
    "content": "Kwanza, nataka kumpongeza Mwenyekiti wa Kamati hii, Mhe. Kizito, kwa kazi safi ambayo ameifanya. Mhe. Naibu Spika wa Muda, mimi pia ni mmoja wa wanakamati ya Utangazaji na Shughuli za Bunge na Maktba. Lakini kabla hata nichangie chochote, kuna jambo ambalo limekuwa likinivunja moyo sana. Sasa ni mwaka wa nne tangu niwe katika Kamati hii. Cha kushangaza ni kwamba Kamati hii ambayo kwa sasa imeleta Hoja hii, ambayo inapongezwa na kila Mbunge, ni Kamati ambayo imechukuliwa kama Kamati hafifu ambayo wanaoadhibiwa na wale ambao wanaonekana kwamba hawafai kuwa katika Kamati kubwa kubwa huletwa upande huu. Hata tunapozungumza saa hii, ni juzi tu ambapo Wenyekiti wa Kamati kadhaa, kwa sababu ya malumbano waliokuwa nayo ndani ya vyama vyao, walitolewa kule na kutupwa huku. Walikuja na ule msimamo wakifiria kuwa hii ni Kamati ambayo haina mwelekeo. Lakini tazama ile kazi ambayo Mhe. Kizito na Wabunge wake wameifanya."
}