GET /api/v0.1/hansard/entries/1069975/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1069975,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1069975/?format=api",
    "text_counter": 165,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi South, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Ken Chonga",
    "speaker": {
        "id": 13374,
        "legal_name": "Richard Ken Chonga Kiti",
        "slug": "richard-ken-chonga-kiti"
    },
    "content": "Kusema kweli kabisa, sisi sote tunafahamu kuwa Bunge ndio mahali ambapo sheria na mwelekeo wa tasasi za Serikali zote hutoka. Iwe ni mahakama au hospitali, kila kitu lazima kiweze kutungwa kama sheria kupitia Bunge hili. La kushangaza ni kwamba katika yote yanayoshughulikiwa katika Bunge hili hakuna lolote ambalo mwananchi analifahamu. Ninapongeza Hoja hii na hatua iliyochukuliwa. Kwanza kabisa, linalonitia moyo ni mbali na kuwa kazi na jitihada za Wabunge kwenye Kamati na kwenye Bunge, pia mwananchi wa kawaida ataweza kuelewa ni kitu kipi kinaendelea Bungeni. Mbali na michango yetu, mwananchi ataweza kufahamu mambo ambayo yanaendelea Bungeni pia."
}