GET /api/v0.1/hansard/entries/1071659/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1071659,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1071659/?format=api",
    "text_counter": 281,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, jambo la pili ni kuipongeza Bunge ya Kaunti ya Wajir kwa kuweza kufanya uchunguzi na kuleta mashtaka haya mbele ya Kamati na Bunge la Seneti, na wakaweza kudhibitisha. Ijapokuwa wameweza kudhibitisha shtaka moja peke yake. Bw. Spika nimeipitia ripoti hii kwa mtazamo fagia, yaani kwa haraka haraka, na nimeona kwamba baadhi ya yale mashtaka ambayo yaliweza kuwasilishwa mbele ya Bunge hili yaliweza kudhibitishwa ijapokuwa Kamati iliweza kuwa na uamuzi tofauti. Mashtaka yote ambayo yalifikishwa mbele ya Bunge la Seneti ni mashtaka ambayo ni magumu sana ama ni serious sana, kiasi ambacho kinaweza kumpeleka nyumbani gavana wa Wajir. Tukiangalia shtaka la kwanza linalohusu kutoajibika katika matumizi ya rasilimali za fedha za Bunge la Kaunti ya Wajir kinyume na vifungu vya 201(a) na 183 vya Katiba yetu na sheria ya 149 and 169 vya Public Finance Management(PFM) Act, 2012. Ijapokuwa mashtaka haya hayakuweza kuthibitishwa, ni wazi kwamba ushahidi ulikuwapo wa kuhukumu au kupata na hatia Gavana huyu kuhusiana na swala hilo."
}