GET /api/v0.1/hansard/entries/1071772/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1071772,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1071772/?format=api",
"text_counter": 20,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taita Taveta CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Haika Mizighi",
"speaker": {
"id": 13274,
"legal_name": "Lydia Haika Mnene Mizighi",
"slug": "lydia-haika-mnene-mizighi"
},
"content": " Asante Mheshimiwa Spika kwa kunipa fursa hii. Nataka kuchukua fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Jessica. Kwa kweli, jambo hili la wanyamapori limekuwa kero kwetu sisi tukiwa pale Taita Taveta. Mbuga ile ya wanyama ya Tsavo imewapatia watu wetu changamoto kwasababu ya kuuliwa na wanyama, mashamba kuharibiwa na mifugo kuliwa na wanyama. Ni wakati kweli jambo hili liweze kuchukuliwa kwa dharura na tupate suluhisho. Maswala haya tumeyaongelea sana hapa Mheshimiwa Spika na ni wakati sasa tunataka kuona ya kwamba tumesaidika. Asante kwa kunipa hii fursa na namuunga mkono."
}