GET /api/v0.1/hansard/entries/1071774/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1071774,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1071774/?format=api",
    "text_counter": 22,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM-K",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": {
        "id": 13509,
        "legal_name": "Danson Mwashako Mwakuwona",
        "slug": "danson-mwashako-mwakuwona"
    },
    "content": " Asante Sana Mheshimiwa Spika. Nami nataka kuunga mkono Maombi yaliyoletwa na wakaazi wa Makueni. Ni kweli Mheshimiwa Spika mwenzangu wa Taita Taveta ameongea na mimi nitasema kwa uchache sana kwamba kilichobaki sasa si mazungumzo tu. Tumeongea na KWS kwa muda mrefu. Tumeongea na Wizara kwa muda mrefu, lakini muda wote huo hatujapata nafuu ama afueni katika maswala haya. Tumeona ni watu ambao wanasema mambo ambayo hawatekelezi. Kule kwangu Wundanyi kuna sehemu inaitwa Kishushe. Wiki iliyopita shule sita zilivamiwa na ndovu, matanki ambayo tumenunua na pesa za NG-CDF yakabomolewa. Jana nilikuwa kwa Ofisi ya PS kumuliza ni vipi wanaweza angalau kufidia matanki yale maanake shule zimefunguliwa na ndio wazazi hawajaruhusu watoto wao kwenda shuleni kwa uoga wa ndovu. Mheshimiwa Spika, Ndovu wa siku hizi ni kama kidogo nao pia wamepiga hatua ya Karne ya 21. Kwasababu gani? Kule kwangu wanakunywa maji kwa matanki kwa juu halafu maji yakipungua na mikono yao haifiki kwa maji, wanayabomoa ndiyo wayafikie hayo maji. Utakuta kwamba nina matanki karibu sita. Ijumaa iliyopita nilikuwa kule. Sasa wamefika mahali ambapo wanatoboa mabati ya nyumba ili wachungulie ndani ama waingize mikono waangalie kama kuna chakula ama chochote. Mheshimiwa Spika, tuna tatizo na mimi naomba hivi: Tunapoangazia maswala ya wanyamapori kuvamia mashamba na mifugo na maisha ya wananchi, tusiangalie sana tu ndovu ama simba. Mwenzangu amesema kwake ni ndege. Sasa kuna tatizo lingine sugu. Nilileta Swali ambalo lilijibiwa na Waziri lakini halikujibiwa mwafaka. Mheshimiwa Spika, kuna tumbiri kwangu milimani ambao wanasumbua na huku chini ni ndovu. Sasa tunaomba tu Wizara ichukulie mambo haya kwa uzito. Mwisho, kila mara The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}